Sasisho la EA SPORTS FC™ Mobile 26 Update limefika! Sherehekea msimu wa soka wa 2025/2026 na ufurahie mojawapo ya masasisho yetu makubwa zaidi kuwahi kutokea. Sasisho hili la kipekee limechochewa na mashabiki ili kukupa uzoefu bora wa mpira wa miguu.
Jijumuishe kikamilifu katika ulimwengu halisi wa soka na FC Mobile, ambapo ndoto zako za kuunda kikosi cha klabu bingwa zinatimia. Chagua klabu yoyote kutoka Ligi Kuu ya Uingereza au LALIGA EA SPORTS, ikiwemo Liverpool na Real Madrid, na ujipime katika Mfumo wa Changamoto za Klabu za PVP. Kusanya kadi za wachezaji nyota kama Jude Bellingham, Virgil van Dijk, Cole Palmer, au magwiji mashuhuri kama David Beckham, Ronaldinho, Zinedine Zidane, na Zlatan Ibrahimović, ili kujenga Timu Yako Bora ya Soka. FC Mobile inakuletea mashindano makubwa zaidi duniani, ligi maarufu, na zaidi ya wachezaji 19,000 kutoka timu 690 katika ligi 35, ikiwemo Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League).
Funga mabao ya kuvutia na wachezaji bora kabisa duniani huku ukiipandisha hadhi timu yako ya nyota wa soka. Shiriki Ligi na ushirikiane na wachezaji wenzako kushindana katika mashindano mbalimbali na kujikusanyia zawadi nyingi zaidi. Pigania kupanda viwango katika mifumo mbalimbali ya mchezo wa soka wa PvP, ikiwemo Changamoto za Klabu, 1v1 H2H, VS Attack, na Mfumo wa Meneja wa Soka. Ongeza kasi ya kujipatia zawadi kupitia Mazoezi ya Kila Siku, Jukumu Maalum, na Mafanikio unayoyatimiza. Jipime dhidi ya washindani katika mechi za Head to Head PvP ili kupanda viwango vya Ligi na kujipatia zawadi kila wiki kutokana na nafasi yako kwenye Ubao wa Wanaoongoza.
Furahia maboresho halisi ya uchezaji yanayoleta uhalisia mpya uwanjani, ikiwemo mifumo mipya ya kimbinu ya kuipanga timu, na mfumo uliokamilika zaidi wa kupiga pasi unaohakikisha usahihi na udhibiti wa hali ya juu. Kuhuishwa kwa uhalisia wa wachezaji kunafanya sifa na mbinu zao za kucheza zionekane wazi kulingana na uchezaji wao halisi. Pia, furahia marekebisho yaliyolenga mashabiki kama vile uboreshaji wa utambuzi wa makosa ya mwamuzi. Pamoja na hayo, tazama FCM TV kwa miongozo ya mchezo, matangazo ya moja kwa moja ya FCM LIVE, na maudhui ya mechi za soka kutoka ligi kubwa duniani kama Ligi Kuu ya Uingereza na LALIGA. Klabu ni Yako, Popote. Cheza mchezo wa dunia na uwapate nyota wakubwa wa soka na magwiji kupitia sasisho la 26 la EA SPORTS FC™ Mobile.